Articles liés à Nyayo Za Obama: Ni Rajua Za Ujasiri

Nyayo Za Obama: Ni Rajua Za Ujasiri - Couverture souple

Sanifu, Kiswahili

9781483669397: Nyayo Za Obama: Ni Rajua Za Ujasiri

Synopsis

Katika Nyayo za Obama msomaji atasoma juu ya mambo makuu matatu: maisha ya rais Barack Husein Obama kuanzia kwa wazazi wake na jinsi walivyokutana, hitilafu zilizowatenganisha, utoto wake na hadi hapo aliko kwenye kilele cha siasa ; nchi ya Marekani iliyompa fursa, hasa kuhusu uanuwai wa watu wake, siasa yake, na sifa zake mashuhuri za masoko makubwa ya kimataifa na hisani yake kwa nchi zingine; na msomaji atamaizi nafasi pekee lugha ya Kiswahili iliyo nayo katika kufungamanisha jumuia za mataifa ya Afrika ambayo mengi bado yanatumia lugha geni kwenye fasihi rasmi za kisiasa na kisheria, na pia ni lugha pekee ambayo vyanzo vyake ni anuwai ya kutosha kuzungumzwa kote barani. Mwishowe, kuna orodha ya msamiati mpya uliotumika katika fasihi kwa minajili ya kuneemesha welekevu wa mada za karne ya mitandao na utandawazi.

Les informations fournies dans la section « Synopsis » peuvent faire référence à une autre édition de ce titre.

Biographie de l'auteur

Safari Ohumay ni Mmarekani mzaliwa wa Tanzania mashambani katika kijiji cha Bashay Mkoani Manyara. Kabla ya makamo ya miaka 30 alikuja Marekani jijini Washington D.C. alikoajiriwa na Benki Kuu ya Dunia mnamo mwaka 1978. Kwa miaka 18 iliyofuata alikuwa msimamizi wa miradi na programu za maendeleo ya miji na muundombinu katika nchi kadhaa za bara la Asia zikiwemo, Indonesia, Srilanka, Bangladeshi, Burma, Papua New Guinea, Nepal na Pakistan. Katika bara la Afrika aliwahi kuhusika na uchanganuzi wa awali wa miradi katika nchi za Swaziland na Malawi, na hapo baadaye alihusika na miradi ya utalii katika nchi ya Kenya. Safari anaishi katika kitongoji moja cha jiji la Washington kwa upande wa jimbo la Maryland. Baada ya kurudi kutoka Afghanistan alikokuwa akisimamia programu za U.S.A.I.D. chini ya mwavuli wa usalama wa majeshi ya Marekani, alianza kufunza Kiswahili kwa watumishi wa serikali na wanajeshi wa idara kadha kupitia kwenye mikataba na vituo vya kufundisha lugha. Safari alisoma shule za Tanzania, akapata shahada ya kwanza katika chuo kikuu cha DaresSalaam, na shahada ya juu katika chuo kikuu cha Hult Kitengo cha Biashara ya Kimataifa, kilichoko kule Cambridge, Massachusetts, Marekani.

Présentation de l'éditeur

Katika Nyayo za Obama msomaji atasoma juu ya mambo makuu matatu: maisha ya rais Barack Husein Obama kuanzia kwa wazazi wake na jinsi walivyokutana, hitilafu zilizowatenganisha, utoto wake na hadi hapo aliko kwenye kilele cha siasa ; nchi ya Marekani iliyompa fursa, hasa kuhusu uanuwai wa watu wake, siasa yake, na sifa zake mashuhuri za masoko makubwa ya kimataifa na hisani yake kwa nchi zingine; na msomaji atamaizi nafasi pekee lugha ya Kiswahili iliyo nayo katika kufungamanisha jumuia za mataifa ya Afrika ambayo mengi bado yanatumia lugha geni kwenye fasihi rasmi za kisiasa na kisheria, na pia ni lugha pekee ambayo vyanzo vyake ni anuwai ya kutosha kuzungumzwa kote barani. Mwishowe, kuna orodha ya msamiati mpya uliotumika katika fasihi kwa minajili ya kuneemesha welekevu wa mada za karne ya mitandao na utandawazi.

Les informations fournies dans la section « A propos du livre » peuvent faire référence à une autre édition de ce titre.