Noah Henry: Hadithi ya Upinde wa Mvua - Couverture souple

Sobel Lederman, Deana

 
9781636070223: Noah Henry: Hadithi ya Upinde wa Mvua

Synopsis

Kama siku yoyote nyingine, Noah Henry anajitayarisha kwenda shuleni-lakini, wazazi wake wanamwambia kwamba shule yake imefungwa. Zaidi ya hilo, bustani ya wanyama pia imefungwa na hataweza kucheza na rafiki zake wanaoishi mle. Mambo hayabadiliki hata wakati Noah na kaka yake mdogo wananawisha mikono yao kama walivyoambiwa na walimu wao. Lakini, wakati Noah na familia yake wanapoondoka kwenda matembezini, anagundua ya kwamba rafiki zake walikuwa wamechora pinde za mvua na kuziweka kwenye madirisha yao, na anatambua ya kwamba rafiki zake pia hawana hakika kuhusu siku zijazo, na ya kwamba siku moja yeye na rafiki zake watacheza pamoja tena.


Les informations fournies dans la section « Synopsis » peuvent faire référence à une autre édition de ce titre.

À propos de l'auteur

Deana Sobel Lederman ni mwandishi na mchoraji. Bibi yake alikuwa mchoraji ambaye alisomea kwenye chuo kiitwacho The Art Students League of New York. Alimfundisha Deana kuhusu uchoraji wakati Deana alikuwa mchanga sana, na mamake Deana pia alimhimiza kuchora kutoka wakati Deana alikuwa mchanga. Deana alichora kitabu chake cha kwanza cha ucheshi kinachoitwa The Wacky Couples wakati alikuwa na miaka minane, na baadaye alikuwa mchoraji mkuu wa gazeti la wanafunzi wa UC Berkeley na msanii aliyechapishwa. Baadaye, alisomea kuhusu sheria ya hakimiliki kwenye chuo kikuu cha sheria. Ameishi New York City; Berkeley, California; London, England; na Cambridge, Massachusetts. Deana alikulia katika mji wa San Diego, California, na hapo ndipo anapoishi pamoja na mume wake na watoto wake wawili.

Les informations fournies dans la section « A propos du livre » peuvent faire référence à une autre édition de ce titre.